Biblia Habari Njema

Yohane 10:12-20 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwamwitu anakuja, huwaacha kondoo na kukimbia, kisha mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya.

13. Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu.

14. Mimi ni mchungaji mwema. Nawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi,

15. kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Mimi nayatoa maisha yangu kwa ajili yao.

16. Tena ninao kondoo wengine ambao hawamo zizini humu. Inanibidi kuwaleta hao pia, nao wataisikia sauti yangu, na kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.

17. “Baba ananipenda kwani nautoa uhai wangu ili nipate kuupokea tena.

18. Hakuna mtu anayeninyanganya uhai wangu; mimi nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye.”

19. Kukawa tena na mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya.

20. Wengi wao wakasema, “Ana pepo; tena ni mwendawazimu! Ya nini kumsikiliza?”