Biblia Habari Njema

Yohane 10:17-20 Biblia Habari Njema (BHN)

17. “Baba ananipenda kwani nautoa uhai wangu ili nipate kuupokea tena.

18. Hakuna mtu anayeninyanganya uhai wangu; mimi nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye.”

19. Kukawa tena na mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya.

20. Wengi wao wakasema, “Ana pepo; tena ni mwendawazimu! Ya nini kumsikiliza?”