Biblia Habari Njema

2 Wafalme 19:25-31 Biblia Habari Njema (BHN)

25. ‘Je, hujasikia,kwamba nilipanga jambo hili tangu awali?Ninachotekeleza sasa nilikipanga zamani.’Nilikuweka uijenge miji yenye ngomekwa rundo la magofu.

26. Wakazi wake wakiwa wameishiwa nguvu,wametishika na kufadhaika,wamekuwa kama mimea ya shambani,kama majani yasiyo na nguvu.Kama majani yaotayo juu ya paa;yakaukavyo kabla ya kukua.

27. Najua kuketi kwako,na kuamka kwakonako kuingia kwako;nayo mipango yako dhidi yangu.

28. Kwa vile umefanya mipango dhidi yanguna nimeusikia ufidhuli wako,nitatia ndoana yangu puani mwako,na lijamu yangu kinywani mwako.Nitakurudisha njia ileile uliyojia.”

29. Kisha Isaya akamwambia mfalme Hezekia, “Na hii ndio itakuwa ishara kwako Hezekia: Mwaka huu na mwaka ujao mtakula kinachomea chenyewe bila kupandwa. Lakini katika mwaka wa tatu mtapanda na kuvuna mavuno; mtapanda mizabibu na kula matunda yake.

30. Wale watakaobaki katika ukoo wa Yuda wataongezeka na kuwa wengi kama vile mti unavyotoa mizizi yake udongoni na kuzaa matunda juu.

31. Maana kutakuwako watu watakaosalia huko Yerusalemu; naam, huko mlimani Siyoni kutakuwako watu wachache watakaosalimika; maana Mwenyezi-Mungu amedhamiria kukamilisha hayo.