Biblia Habari Njema

Yohane 9:31-37 Biblia Habari Njema (BHN)

31. Tunajua kwamba Mungu hawasikilizi watu wenye dhambi, ila humsikiliza yeyote mwenye kumcha na kutimiza mapenzi yake.

32. Tangu mwanzo wa ulimwengu haijasikika kwamba mtu ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu.

33. Kama mtu huyu hakutoka kwa Mungu, hangeweza kufanya chochote!”

34. Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa na kulelewa katika dhambi; unawezaje kutufundisha sisi?” Basi, wakamfukuza sunagogini.

35. Yesu alisikia kwamba walikuwa wamemfukuza sunagogini. Basi, alipomkuta akamwuliza, “Je, wewe unamwamini Mwana wa Mtu?”

36. Huyo mtu akajibu, “Mheshimiwa, niambie yeye ni nani, ili nipate kumwamini.”

37. Yesu akamwambia, “Umekwisha mwona, naye ndiye anayesema nawe sasa.”