Biblia Habari Njema

Yohane 6:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Baada ya hayo, Yesu alivuka ziwa Galilaya (au ziwa Tiberia).

2. Umati mkubwa wa watu ulimfuata kwa sababu watu hao walikuwa wameona ishara alizokuwa akifanya kwa kuwaponya wagonjwa.

3. Yesu alipanda mlimani, akaketi pamoja na wanafunzi wake.

4. Sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka ilikuwa imekaribia.

5. Basi, Yesu alipotazama na kuona umati wa watu ukija kwake, alimwambia Filipo, “Tununue wapi mikate ili watu hawa wapate kula?”