Biblia Habari Njema

Yohane 5:39-47 Biblia Habari Njema (BHN)

39. Nyinyi huyachunguza Maandiko Matakatifu mkidhani kwamba ndani yake mtapata uhai wa milele; na kumbe maandiko hayohayo yananishuhudia!

40. Hata hivyo, nyinyi hamtaki kuja kwangu ili mpate uhai.

41. “Shabaha yangu si kupata sifa kutoka kwa watu.

42. Lakini nawajua nyinyi, najua kwamba upendo kwa Mungu haumo mioyoni mwenu.

43. Mimi nimekuja kwa mamlaka ya Baba yangu, lakini hamnipokei; bali mtu mwingine akija kwa mamlaka yake mwenyewe, mtampokea.

44. Mwawezaje kuamini, hali nyinyi mnapenda kupokea sifa kutoka kwenu nyinyi wenyewe, wala hamtafuti sifa kutoka kwake yeye aliye peke yake Mungu?

45. Msifikiri kwamba mimi nitawashtaki kwa Baba. Mose ambaye nyinyi mmemtumainia ndiye atakayewashtaki.

46. Kama kweli mngemwamini Mose, mngeniamini na mimi pia, maana Mose aliandika juu yangu.

47. Lakini hamyaamini yale aliyoandika; mtawezaje basi, kuamini maneno yangu?”