Biblia Habari Njema

Yohane 3:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kulikuwa na kiongozi mmoja Myahudi, wa kikundi cha Mafarisayo, jina lake Nikodemo.

2. Siku moja Nikodemo alimwendea Yesu usiku, akamwambia, “Rabi, tunajua kwamba wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, maana hakuna mtu awezaye kufanya ishara unazozifanya Mungu asipokuwa pamoja naye.”

3. Yesu akamwambia, “Kweli nakuambia, mtu asipozaliwa tena hataweza kuuona ufalme wa Mungu.”

4. Nikodemo akamwuliza, “Mtu mzima awezaje kuzaliwa tena? Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake na kuzaliwa tena!”

5. Yesu akamjibu, “Kweli nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu.

6. Mtu huzaliwa kimwili kwa baba na mama, lakini huzaliwa kiroho kwa Roho.

7. Usistaajabu kwamba nimekuambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya.

8. Upepo huvuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda. Ndivyo ilivyo kwa mtu aliyezaliwa kwa Roho.”

9. Nikodemo akamwuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?”

10. Yesu akamjibu, “Je, wewe ni mwalimu katika Israeli na huyajui mambo haya?