Biblia Habari Njema

Yohane 20:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza, Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi.

2. Basi, akaenda mbio hadi kwa Petro na yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, “Wamemwondoa Bwana kaburini, na wala hatujui walikomweka.”

3. Petro pamoja na yule mwanafunzi mwingine wakaenda kaburini.

4. Wote wawili walikimbia lakini yule mwanafunzi mwingine alikimbia mbio kuliko Petro, akatangulia kufika kaburini.

5. Alipoinama na kuchungulia ndani, aliona sanda, lakini hakuingia ndani.

6. Simoni Petro naye akaja akimfuata, akaingia kaburini; humo akaona sanda,

7. na kile kitambaa alichofungwa Yesu kichwani. Hicho kitambaa hakikuwekwa pamoja na hiyo sanda, bali kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa mahali peke yake.

8. Kisha yule mwanafunzi mwingine aliyetangulia kufika kaburini, akaingia pia ndani, akaona, akaamini. (