Biblia Habari Njema

Yohane 15:7-12 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, basi, ombeni chochote mtakacho nanyi mtapewa.

8. Baba yangu hutukuzwa kama mkizaa matunda mengi na kuwa wanafunzi wangu.

9. Mimi nimewapenda nyinyi kama vile Baba alivyonipenda mimi. Kaeni katika pendo langu.

10. Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama vile nami nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.

11. Nimewaambieni mambo haya ili furaha yangu ikae ndani yenu, na furaha yenu ikamilike.

12. Hii ndiyo amri yangu: Pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi.