Biblia Habari Njema

Yohane 11:9-21 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Yesu akajibu, “Je, saa za mchana si kumi na mbili? Basi, mtu akitembea mchana hawezi kujikwaa kwa kuwa anauona mwanga wa ulimwengu huu.

10. Lakini mtu akitembea usiku atajikwaa kwa maana mwanga haumo ndani yake.”

11. Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, akawaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini mimi nitakwenda kumwamsha.”

12. Wanafunzi wake wakamwambia, “Bwana, ikiwa amelala, basi atapona.”

13. Wao walidhani kwamba alikuwa amesema juu ya kulala usingizi, kumbe alikuwa amesema juu ya kifo cha Lazaro.

14. Basi, Yesu akawaambia waziwazi, “Lazaro amekufa;

15. lakini nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini. Haya, twendeni kwake.”

16. Thoma (aitwaye Pacha) akawaambia wanafunzi wenzake, “Twendeni nasi tukafe pamoja naye!”

17. Yesu alipofika huko alikuta Lazaro amekwisha kaa kaburini kwa siku nne.

18. Kijiji cha Bethania kilikuwa karibu na Yerusalemu, umbali upatao kilomita tatu.

19. Wayahudi wengi walikuwa wamefika kwa Martha na Maria kuwafariji kwa kifo cha kaka yao.

20. Basi, Martha aliposikia kwamba Yesu alikuwa anakuja, akaenda kumlaki; lakini Maria alibaki nyumbani.

21. Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!