Biblia Habari Njema

Yohane 11:25-29 Biblia Habari Njema (BHN)

25. Yesu akamwambia, “Mimi ndimi ufufuo na uhai. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi;

26. na kila anayeishi na kuniamini, hatakufa kamwe. Je, waamini hayo?”

27. Martha akamwambia, “Ndiyo Bwana! Mimi naamini kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.”

28. Baada ya kusema hayo, Martha alikwenda kumwita Maria, dada yake, akamwambia faraghani, “Mwalimu yuko hapa, anakuita.”

29. Naye aliposikia hivyo, akainuka mara, akamwendea Yesu.