Biblia Habari Njema

Yohane 11:20-26 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Basi, Martha aliposikia kwamba Yesu alikuwa anakuja, akaenda kumlaki; lakini Maria alibaki nyumbani.

21. Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!

22. Lakini najua kwamba hata sasa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa.”

23. Yesu akamwambia, “Kaka yako atafufuka.”

24. Martha akamjibu, “Najua kwamba atafufuka wakati wa ufufuo, siku ya mwisho.”

25. Yesu akamwambia, “Mimi ndimi ufufuo na uhai. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi;

26. na kila anayeishi na kuniamini, hatakufa kamwe. Je, waamini hayo?”