Biblia Habari Njema

Yohane 10:20-26 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Wengi wao wakasema, “Ana pepo; tena ni mwendawazimu! Ya nini kumsikiliza?”

21. Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mwenye pepo. Je, pepo anaweza kuyafumbua macho ya vipofu?”

22. Huko Yerusalemu kulikuwa na sikukuu ya kutabaruku. Wakati huo ulikuwa wa baridi.

23. Naye Yesu akawa anatembea hekaluni katika ukumbi wa Solomoni.

24. Basi, Wayahudi wakamzunguka, wakamwuliza, “Utatuacha katika mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiwe Kristo, basi, tuambie wazi.”

25. Yesu akawajibu, “Nimewaambieni, lakini hamsadiki. Kazi ninazozifanya mimi kwa jina la Baba yangu zinanishuhudia.

26. Lakini nyinyi hamsadiki kwa sababu nyinyi si kondoo wangu.