Biblia Habari Njema

Yohane 10:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Kweli nawaambieni, yeyote yule asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya na kuingia kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyanganyi.

2. Lakini anayeingia kwa kupitia mlangoni, huyo ndiye mchungaji wa kondoo.

3. Mngojamlango wa zizi humfungulia, na kondoo husikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kila mmoja kwa jina lake, na kuwaongoza nje.

4. Akisha watoa nje huwatangulia mbele, nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake.

5. Kondoo hao hawawezi kumfuata mgeni, bali watamkimbia kwa sababu hawaijui sauti yake.”

6. Yesu aliwaambia mfano huo, lakini wao hawakuelewa alichotaka kuwaambia.

7. Basi, akasema tena, “Kweli nawaambieni, mimi ni mlango wa kondoo.