Biblia Habari Njema

Mhubiri 8:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Nani aliye kama mwenye hekima?Nani ajuaye hali halisi ya vitu?Hekima humletea mtu tabasamu,huubadilisha uso wake mwenye huzuni.

2. Tii amri ya mfalme, kwa sababu ya kiapo chako kitakatifu.

3. Usifanye haraka kuondoka mbele yake; wala usiwe na kiburi juu ya jambo baya, maana mfalme hufanya apendavyo.

4. Amri ya mfalme ni kauli ya mwisho; nani athubutuye kumwuliza, “Unafanya nini?”