Biblia Habari Njema

Mhubiri 11:2-5 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Wagawie watu saba hata wanane sehemu yako,maana, hujui balaa litakalofika duniani.

3. Mawingu yakijaa maji, mvua hunyesha;mti ukiangukia kusini au kaskazini,hapo uangukiapo ndipo ulalapo.

4. Anayengoja upepo hatapanda mbegu,anayesubiri mawingu yatoweke, hatavuna kitu.

5. Usivyojua jinsi uhai unavyoingia katika mifupa ya mtoto tumboni mwa mamake, kadhalika huwezi kuelewa matendo ya Mungu, ambayo hufanya kila kitu.