Biblia Habari Njema

Mhubiri 11:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Jishughulishe na biasharahata kama kwa kubahatisha;yawezekana baadayeukapata chochote kile.

2. Wagawie watu saba hata wanane sehemu yako,maana, hujui balaa litakalofika duniani.

3. Mawingu yakijaa maji, mvua hunyesha;mti ukiangukia kusini au kaskazini,hapo uangukiapo ndipo ulalapo.

4. Anayengoja upepo hatapanda mbegu,anayesubiri mawingu yatoweke, hatavuna kitu.

5. Usivyojua jinsi uhai unavyoingia katika mifupa ya mtoto tumboni mwa mamake, kadhalika huwezi kuelewa matendo ya Mungu, ambayo hufanya kila kitu.

6. Panda mbegu asubuhi na jioni usiache kupanda, maana, hujui zipi zitaota; za asubuhi, za jioni, au zote zitakuwa nzuri.