Biblia Habari Njema

Matendo 20:33-37 Biblia Habari Njema (BHN)

33. Mimi sikutamani hata mara moja fedha, wala dhahabu, wala nguo za mtu yeyote.

34. Mnajua nyinyi wenyewe kwamba nimefanya kazi kwa mikono yangu mwenyewe, ili kujipatia mahitaji yangu na ya wenzangu.

35. Nimekuwa nikiwapeni daima mfano kwamba kwa kufanya kazi mithili hiyo tunapaswa kuwasaidia walio dhaifu, tukikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe: ‘Heri zaidi kutoa kuliko kupokea.’”

36. Baada ya kusema hayo, Paulo alipiga magoti pamoja nao wote, akasali.

37. Wote walikuwa wanalia, na kumwaga kwa kumkumbatia na kumbusu.