Biblia Habari Njema

Matendo 20:25-27 Biblia Habari Njema (BHN)

25. “Nimepita miongoni mwenu nyote nikiuhubiri ufalme wa Mungu. Sasa lakini, najua hakuna hata mmoja wenu atakayeniona tena.

26. Hivyo, leo hii ninawathibitishieni rasmi kwamba ikijatokea akapotea mmoja wenu, mimi sina lawama yoyote.

27. Kwa maana sikusita hata kidogo kuwatangazieni azimio lote la Mungu.