Biblia Habari Njema

Matendo 2:32-36 Biblia Habari Njema (BHN)

32. Basi, Mungu alimfufua huyo Yesu na sisi sote ni mashahidi wa tukio hilo.

33. Yesu alipokwisha pandishwa na kuwekwa na Mungu upande wake wa kulia, akapokea kutoka kwake Baba yule Roho Mtakatifu ambaye alituahidi, ametumiminia huyo Roho. Hicho ndicho mnachoona sasa na kusikia.

34. Maana Daudi mwenyewe, hakupanda mpaka mbinguni; ila yeye alisema:‘Bwana alimwambia Bwana wangu:Keti upande wangu wa kulia,

35. hadi niwafanye adui zako kiti cha miguu yako.’

36. “Watu wote wa Israeli wanapaswa kufahamu kwa hakika kwamba huyo Yesu mliyemsulubisha, ndiye huyo ambaye Mungu amemfanya kuwa Bwana na Kristo.”