Biblia Habari Njema

Matendo 2:27-34 Biblia Habari Njema (BHN)

27. maana hutaiacha roho yangu kuzimu,wala kumruhusu mtakatifu wako aoze.

28. Umenionesha njia za uhai,umenijaza furaha kwa kuwako kwako!’

29. “Ndugu zangu, napenda kuwaambieni waziwazi juu ya mambo yaliyompata Daudi, babu yetu. Yeye alikufa, akazikwa, tena kaburi lake liko papa hapa petu mpaka leo.

30. Lakini kwa vile Daudi alikuwa nabii, alijua kuwa Mungu alimwapia kiapo kwamba atamtawaza mmoja wa uzawa wake kuwa mfalme mahali pake.

31. Daudi aliona kabla mambo yatakayofanywa na Mungu na hivyo akasema juu ya ufufuo wa Kristo wakati aliposema: ‘Hakuachwa kuzimu, mwili wake haukuoza.’

32. Basi, Mungu alimfufua huyo Yesu na sisi sote ni mashahidi wa tukio hilo.

33. Yesu alipokwisha pandishwa na kuwekwa na Mungu upande wake wa kulia, akapokea kutoka kwake Baba yule Roho Mtakatifu ambaye alituahidi, ametumiminia huyo Roho. Hicho ndicho mnachoona sasa na kusikia.

34. Maana Daudi mwenyewe, hakupanda mpaka mbinguni; ila yeye alisema:‘Bwana alimwambia Bwana wangu:Keti upande wangu wa kulia,