Biblia Habari Njema

Matendo 11:4-9 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Hapo Petro akawaeleza kinaganaga juu ya yale yaliyotendeka tangu mwanzo:

5. “Siku moja nikiwa nasali mjini Yopa, niliona maono; niliona kitu kama shuka kubwa ikishushwa chini kutoka mbinguni ikiwa imeshikwa pembe zake nne, ikawekwa kando yangu.

6. Nilichungulia ndani kwa makini nikaona wanyama wenye miguu minne, wanyama wa mwituni, wanyama watambaao na ndege wa angani.

7. Kisha nikasikia sauti ikiniambia: ‘Petro amka, chinja, ule.’

8. Lakini mimi nikasema: ‘La, Bwana; maana chochote kilicho najisi au kichafu hakijapata kamwe kuingia kinywani mwangu.’

9. Ile sauti ikasikika tena kutoka mbinguni: ‘Usiviite najisi vitu ambavyo Mungu amevitakasa.’