Biblia Habari Njema

Luka 8:8-12 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Nyingine zilianguka katika udongo mzuri, zikaota na kuzaa asilimia mia.” Baada ya kusema hayo, akapaza sauti, akasema, “Mwenye masikio na asikie!”

9. Wanafunzi wake Yesu wakamwuliza maana ya mfano huo.

10. Naye akajibu, “Nyinyi mmejaliwa kujua siri za ufalme wa Mungu, lakini hao wengine sivyo; ila hao huambiwa kwa mifano, ili wakitazama wasiweze kuona, na wakisikia wasifahamu.

11. “Basi, maana ya mfano huu ni hii: Mbegu ni neno la Mungu.

12. Zile zilizoanguka njiani zinaonesha watu wale wanaosikia lile neno, halafu Ibilisi akaja na kuliondoa mioyoni mwao wasije wakaamini wakaokoka.