Biblia Habari Njema

Luka 24:37-44 Biblia Habari Njema (BHN)

37. Wakashtuka na kushikwa na hofu wakidhani wameona mzimu.

38. Lakini yeye akawaambia, “Kwa nini mnafadhaika? Mbona mnakuwa na mashaka mioyoni mwenu?

39. Angalieni mikono na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe. Nipapaseni mkaone, maana mzimu hauna mwili na mifupa kama mnionavyo.”

40. Baada ya kusema hayo, akawaonesha mikono na miguu.

41. Wakiwa bado katika hali ya kutosadiki kwa sababu ya furaha yao, na wakiwa wanastaajabu, akawauliza, “Mnacho chakula chochote hapa?”

42. Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa.

43. Akakichukua, akala, wote wakimwona.

44. Halafu akawaambia, “Hii ndiyo maana ya maneno niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi: Kwamba ilikuwa lazima kukamilisha yote yaliyoandikwa juu yangu katika sheria ya Mose na katika vitabu vya manabii na katika kitabu cha Zaburi.”