Biblia Habari Njema

Luka 24:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Jumapili, alfajiri na mapema, wale wanawake walikwenda kaburini wakichukua yale manukato waliyotayarisha.

2. Walikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi.

3. Walipoingia ndani, hawakuuona mwili wa Bwana Yesu.

4. Walipokuwa bado wanashangaa juu ya jambo hilo, mara watu wawili waliovaa mavazi yenye kungaa sana, wakasimama karibu nao.

5. Hao wanawake wakaingiwa na hofu, wakainama chini. Ndipo wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai kati ya wafu?