Biblia Habari Njema

Luka 20:11-18 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Yule bwana akamtuma tena mtumishi mwingine; lakini wao wakampiga huyo vilevile na kumtendea vibaya, wakamrudisha mikono mitupu.

12. Akamtuma tena wa tatu; huyu naye, baada ya kumwumiza, wakamfukuza.

13. Yule mwenye shamba akafikiri: ‘Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpenzi; labda watamjali yeye.’

14. Wale wakulima walipomwona tu, wakasemezana: ‘Huyu ndiye mrithi. Basi, tumuue ili urithi wake uwe wetu.’

15. Basi, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu, wakamuua.” Yesu akauliza, “Yule mwenye shamba atawafanya nini hao wakulima?

16. Atakuja kuwaangamiza wakulima hao, na kuwapa wakulima wengine hilo shamba la mizabibu.” Watu waliposikia maneno hayo, walisema: “Hasha! Yasitukie hata kidogo!”

17. Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, “Maandiko haya Matakatifu yana maana gani, basi?‘Jiwe walilokataa waashi,sasa limekuwa jiwe kuu la msingi!’

18. Mtu yeyote akianguka juu ya jiwe hilo atavunjika vipandevipande; na likimwangukia mtu yeyote, litamponda.”