Biblia Habari Njema

Luka 15:15-20 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Akaomba kazi kwa mwananchi mmoja wa huko naye akampeleka shambani mwake kulisha nguruwe.

16. Alitamani kula maganda waliyokula wale nguruwe, ila hakuna mtu aliyempa kitu.

17. Alipoanza kupata akili, akafikiri: ‘Mbona kuna wafanyakazi wengi wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa?

18. Nitarudi kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia.

19. Sistahili hata kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wa wafanyakazi wako.’

20. Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu.