Biblia Habari Njema

Luka 15:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Siku moja, watozaushuru na wenye dhambi wengi walikwenda kumsikiliza Yesu.

2. Mafarisayo na waalimu wa sheria wakaanza kunungunika: “Mtazameni mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi, na tena anakula nao.”

3. Yesu akawajibu kwa mfano:

4. “Hivi, mmoja wenu akiwa na kondoo 100, akigundua kwamba mmoja wao amepotea, atafanya nini? Atawaacha wale tisini na tisa mbugani, na kwenda kumtafuta yule aliyepotea mpaka ampate.

5. Akimpata, atambeba mabegani kwa furaha.