Biblia Habari Njema

Luka 14:32-35 Biblia Habari Njema (BHN)

32. Kama anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo mwingine angali mbali.

33. Vivyo hivyo, basi, hakuna hata mmoja wenu atakayekuwa mwanafunzi wangu kama asipoachilia kila kitu alicho nacho.

34. “Chumvi ni nzuri; lakini ikipoteza ladha yake, itakolezwa na nini?

35. Haifai kitu wala kwa udongo wala kwa mbolea. Watu huitupilia mbali. Mwenye masikio na asikie!”