Biblia Habari Njema

Luka 10:4-10 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Msichukue mfuko wa fedha, mkoba, wala viatu; msimsalimu mtu yeyote njiani.

5. Mkiingia katika nyumba yoyote, kwanza wasalimuni hivi: ‘Amani iwe katika nyumba hii!’

6. Kama akiwako mpenda amani, amani yenu itakaa naye, la sivyo, itawarudieni.

7. Kaeni katika nyumba hiyo mkila na kunywa wanavyowapeni, maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msiende mara nyumba hii mara nyumba ile.

8. Kama mkifika mji fulani na watu wakiwakaribisha, kuleni wanavyowapeni.

9. Ponyeni wagonjwa walioko huko, waambieni watu: ‘Ufalme wa Mungu umekaribia kwenu.’

10. Lakini mkiingia katika mji wowote, wasipowakaribisheni, tokeni; nanyi mpitapo katika barabara zao semeni: