Biblia Habari Njema

Luka 1:41-47 Biblia Habari Njema (BHN)

41. Mara tu Elisabeti aliposikia sauti ya Maria, mtoto mchanga tumboni mwake Elisabeti akaruka. Naye Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu,

42. akasema kwa sauti kubwa, “Umebarikiwa kuliko wanawake wote, naye utakayemzaa amebarikiwa.

43. Mimi ni nani hata mama wa Bwana wangu afike kwangu?

44. Nakuambia, mara tu niliposikia sauti yako, mtoto mchanga tumboni mwangu aliruka kwa furaha.

45. Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale Bwana aliyokuambia.”

46. Naye Maria akasema,“Moyo wangu wamtukuza Bwana,

47. roho yangu inafurahi kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu.