Biblia Habari Njema

2 Wafalme 21:19-24 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; alitawala miaka miwili huko Yerusalemu. Jina la mama yake ni Meshulemethi, binti Haruzi wa Yothba.

20. Alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, kama vile Manase baba yake alivyofanya.

21. Alifuata njia yote aliyoiendea baba yake na kutumikia sanamu ambazo baba yake alizitumikia na kuziabudu.

22. Alimwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zake, hakushika njia ya Mwenyezi-Mungu.

23. Baadaye watumishi wa Amoni walikula njama na kumwua katika ikulu yake.

24. Lakini watu wa Yuda wakawaua wote waliomuua Amoni. Kisha watu hao wa Yuda wakamtawaza Yosia mwanawe mahali pake.