1. Nzi waliokufa husababisha marashi kunuka;upumbavu kidogo hubatilisha hekima na heshima.
2. Moyo wa mwenye hekima humwongoza kutenda yaliyo sawa;lakini mtu mpumbavu moyo wake humpotosha.
3. Hata apitapo njiani, mpumbavu hutambulikana hivyo,humjulisha kila mtu kwamba yeye ni mpumbavu.
4. Mtawala akikuwakia hasira, usijiuzulu;makosa makubwa huweza kufutwa ukiwa mnyenyekevu.
5. Kuna uovu niliogundua hapa duniani, uovu unaosababishwa na watawala:
6. Kwamba wapumbavu wanapewa kazi za madaraka ya juu, na matajiri wanachukua nafasi za mwisho.
7. Nimeona watumwa wanapanda farasi, na wakuu wanatembea kwa miguu kama watumwa.